NEWS  

Prayer

Friends 
in the world

Ecumenism
and dialogue

Peace

Solidarity

The Youngest

The Aged

Friends 
on the street

Friends in prison

Eco-solidarity

Mentally disabled
Friends with no boundaries

Movements

Long Live
the Elderly

The Country of the Rainbow

The Friends

Peace People

 

We have prayer:

Rome
 every evening at 20.30 in the Basilica of Santa Maria in Trastevere.
In this church every Saturday at 20.00 and Sunday at 17.30 we celebrate the eucharistic liturgy.

Jumuiya ya Sant’Egidio ilianzishwa mjini Roma mwaka 1968, pindi baada ya kukamilika kwa Mtaguso wa pili wa Vatican. Leo ni familia kubwa ya Walei yenye zaidi ya wanachama 40,000 Roma, nchini Italia na katika nchi zaidi ya 60 duniani kote ambako watu wamejitoa maisha yao kwa ajili ya kueneza Injili na kuwasaidia wengine.

Sant’Egidio ni Jumuiya ya Walei katika Kanisa Katoliki. Jumuiya mbalimbali za Sant’Egidio zilizoenea duniani kote zinashiriki, kufuata na kuishi kwa namna moja malengo na taratibu za Jumuiya hii. Hii hufanya Jumuiya ya Sant’Egidio kufanana popote pale ilipo duniani.

Sala, ndiyo sehemu muhimu zaidi katika maisha ya Jumuiya ya Sant’Egidio kule Roma na pia duniani kote.
Sala ndiyo kielelezo na msingi wa maisha katika Jumuiya hii.

Uenezaji Injili, ndicho kiini cha uhai wa Jumuiya ya Sant’Egidio. Ni jukumu linalowahusu wale wote wanaotafuta kufahamu maana kamili ya maisha yao.

Kuishi Mshikamano na Maskini, katika kujitolea na kuhudumia bila kudai malipo kwa moyo wa kiinjili wa Kanisa ambalo ni “Kanisa kwa ajili ya watu wote, na hasa kwa watu maskini” (Papa Yohane XXIII).

Kukuza Ushirikiano wa Madhehebu, kwa kuishi kirafiki, kusali na kutafuta umoja wa Wakristu wa madhehebu yote duniani kote.

Njia ya Mazungumzo, iliyopendekezwa na Mtaguso wa Pili wa Vatican kama njia ya amani na ushirikiano kati ya dini zote, na pia kama namna ya kuishi na njia ya kutatua migogoro kati ya watu.

Jumuiya hii ina makao yake makuu katika Kanisa la Sant’Egidio mjini Roma, ambapo ndiko jina la Jumuiya limetoka. Tangu mwanzo wake, Jumuiya ya Sant’Egidio imeendelea kudumisha makao yake katika eneo la Trastevere mjini Roma, ikiendesha sala pamoja na kuwapokea maskini na wageni mahujaji.


Links

Select language